Sunday, February 24, 2013

TBC-shirika la utangazaji tanzania latoa msaada kwa watoto-Matukio habari


Matukio na habari za wiki, TBC yawasaida watoto walemavu

tbc-misaada-matukio-habari

Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (katikat) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana kuhusu maktaba hiyo wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam leo. Wengine ni Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mang’enya (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa tatu kushoto) na wafanyakazi wengine wa Vita Foam, TBC na walimu wa shule hiyo.

Shirika la Utangazaji nchini (TBC) pamoja na Kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited, leo wamekabidhi msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 3 kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam. Msaada huo ni sehemu ya marejesho ya faida inayoipata kwa jamii (CSR).

tbc-misaada-matukio-habari 
Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto)


2 comments: